31/01/2026
Waefeso 3:20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya NGUVU itendayo kazi ndani yetu;
NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YAKO;
Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea NGUVU akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
- Nguvu ili mfufua Yesu kutoka Kaburi
- Nguvu Ya kushinda Dhambi
- Nguvu ya kuendelea Hata k**a kuna Changamoto
Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa NGUVU nao wenye nguvu wauteka.
Kuna Nguvu ya Kiungu ikiwa ndani Mwako ndio vitu vinaenda!
Roho Mtakatifu ndio Nguvu, Anatakiwa Awepo ndani yako
Hawezi kukaa mahali ambapo Yesu hajakaribishwa kwanza
Mkiri Yesu! Aingie ndani mwako! Nguvu za kiungu zitakuwa ndani yako!
Una hitaji nguvu kwenye Ukiroho wako
Una hitaji Nguvu kwenye Akili zako
Unahitaji nguvu kwenye mwili wako
Unahitaji nguvu kwenye kufanya maamuzi
Unahitaji nguvu Kutoboa kwenye Utajiri
Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye NGUVU za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, k**a hivi leo.
Nimaombi Yangu, Mungu Akupe Ufunuo zaidi ujue namna ya kupata NGUVU, Kuitunza NGUVU Ufanikiwe kwenye lolote
Ilikuufikisha mzigo sehemu unahitaji nguvu kuuinua
Tunahitaji NGUVU kuweza kufanikiwa katika jambo lolote!
Uwe na ijumaa njema;