Afya Fruits

Afya Fruits HUDUMA ZA KUPATA ELIMU/USHAURI/BIASHARA

30/09/2020

BIDHAA ZENYE KEMIKALI Vs MATUNDA HALISI

Katika urembo kumekuwa na matumizi makubwa ya bidhaa za urembo zinazotengenezwa kwa kemikali ambazo sio salama katika afya ya mtumiaji.

Mtu kutumia sabuni au mafuta yaliyo tengenezwa kwa tunda au mboga mboga pamoja na kemikali na kuacha kula tunda au mboga mboga halisi bila kujua kuwa kemikali zilizopo katika bidhaa anayotumia zina madhara katika afya yake.

Aliyewai kuwa mmoja kati ya watumiaji wa bidhaa za urembo zenye kemikali ndugu Tea Skrjanec aliwai kusema " Nilipoanza safari ya kula matunda na mboga mboga nilijikuta naachana na vitu vyote vya bandia katika maisha yangu.
Niligundua uzuri hauletwi na bidhaa za urembo bali afya bora. Makampuni makubwa ya bidhaa za urembo yanatuhaminisha kununua bidhaa zao kwa kigezo tutapata matokeo mazuri tutakapo tumia bidhaa zao, ukweli ni kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo ni sumu ambazo huwezi kuziona nje ya mwili. Matumizi ya bidhaa hizi za kemikali mwishowe husababisha mwili kuwa na sumu kupita kiasi, na sumu hizi zinahusishwa na kusababisha magonjwa k**a Saratani(kansa),mimba kuharibika,mzio(allergy), uharibifu wa mfumo wa kinga,ngozi kuwa kavu,utasa na uharibifu wa manii.

Katika maisha yangu ya ujana nilikuwa na mawazo ya kuwekeza pesa zangu katika mwili wangu k**a kununua mapambo,vipodozi,nguo,viatu na vitu vingine vya urembo.
Sikujua k**a vitu hivi vilikuwa na sumu ambayo mwisho wa siku zitaniletea madhara."

Uzito mkubwa/Unene kupita kiasi limekuwa tatizo kubwa kwa watoto katika karne hii ya 21.Watoto wamekuwa katika hatari ya...
09/03/2020

Uzito mkubwa/Unene kupita kiasi limekuwa tatizo kubwa kwa watoto katika karne hii ya 21.

Watoto wamekuwa katika hatari ya kupata kisukari na magonjwa ya moyo katika umri mdogo.

Matumizi ya vyakula vya wanga na sukari Ndio chanzo. ( mikate,keki,soda,juisi, chocolate,pizza,Burger, ice cream,pipi n.k)

MPENDE MWANAO

Badala ya soda na keki katika birthday yake mtengenezee salad ya matunda.
Badala juisi mnunulie matunda.

Hili ni gazeti la THE SUN toleo namba 10. Gazeti hili ni la Mei 6, 1871 mwandishi alikuwa anaelezea umuhimu wa kula matu...
26/02/2020

Hili ni gazeti la THE SUN toleo namba 10. Gazeti hili ni la Mei 6, 1871 mwandishi alikuwa anaelezea umuhimu wa kula matunda ili kuongeza damu mwilini, hasa ulaji wa tunda la Tufaa " Apple ".

Bado nina imani kaka zangu Luqman Maloto na Hafidh Kido ipo siku wataandika "ULAJI WA MATUNDA KIAFYA NI MUHIMU" katika taaluma yao.

Bado Watanzania wengi hawafahamu umuhimu wa kula kiafya ( Health eating ) hivyo ni muhimu kuwapa maarifa.

ZABIBI (GRAPES)Katika matunda ambayo ni mazuri na matamu kisha yanafaida nyingi na muhimu basi Zabibu ni moja wapo.Zabib...
24/02/2020

ZABIBI (GRAPES)

Katika matunda ambayo ni mazuri na matamu kisha yanafaida nyingi na muhimu basi Zabibu ni moja wapo.

Zabibu ni tunda ambalo nchini Tanzania huoatikana kwa wingi mkoani Dodoma.

Kuna aina nyingi za zabibu k**a zabibu za kijani, nyekundu, nyeusi, njano na rangi ya pink.
Vitamini k**a C, K, na B6 hupatikana ndani ya zabibu, pia fibers na madini k**a copper, potassium na manganese hupatikana ndani ya zabibu.

Oxidative stress (msongo wa sumu) ni kisababishi cha magonjwa k**a Kisukari, Kansa na ugonjwa wa moyo.
Viondoa sumu vyenye nguvu kubwa ambavyo utumika kuondoa sumu mwilini (oxidative stress) hupatikana kwa wingi kwenye zabibu, hivyo ulaji wa zabibu unatakiwa kuwa mkubwa ili kujikinga na magonjwa hayo.

Moja ya tafiti iliyofanya inaekeza watu 30 walio juu ya umri wa miaka 50 wakila zabibu grams 450 kwa kila mmoja ndani ya siku moja kwa muda wa wiki mbili watakuwa wamejikinga na kansa ya utumbo mkubwa.

Kikombe kimoja cha zabibu kina ujazo wa 288 mg wa madini ya potassium ambayo ulaji wa madini haya ni kinga dhidi ya magonjwa k**a BP ya kupanda ( high blood pressure) na kiharusi (stroke) .

MATUNDA EVENT 2020Hii ni kampeni ya kuhamasisha na kuwaelimisha watu umuhimu wa kula matunda, katika kujenga na kuimaris...
23/02/2020

MATUNDA EVENT 2020
Hii ni kampeni ya kuhamasisha na kuwaelimisha watu umuhimu wa kula matunda, katika kujenga na kuimarisha afya zao.
Sio kwamba watu hawali matunda kila siku, hapana. Watu wanakula kila siku ila tatizo wanakula katika njia ambazo hawawezi pata au kuona faida za matunda hayo kiafya. Hivyo Taasisi ya AFYAFRUITS ACADEMY imekuja na utaratibu wa kuwakutanisha watu sehemu moja kupata elimu juu ya ulaji sahihi wa matunda kiafya na kula matunda yenyewe bila kusahau michezo inayo changamsha akili. Jambo hili tunaliita MATUNDA EVENT.
Novemba 03,2019 katika jiji la Dar es salaam tulifanya uzinduzi wa event https://m.youtube.com/watch?fbclid=IwAR18_XFEyAyDTlkDQuDIWT_sD90ipBpEshNoFWZnyfCJuGdz50ceiG_yzhg&feature=youtu.be&v=Ik_pzH6SdBc basi napenda kusema kuwa 2020 tunaendeleza kile tulicho kianzisha 2019.
DODOMA MATUNDA EVENT.
Kwa wakazi wa Dodoma karibuni sana Mei 30,2020 tutakuwa na tukio muhimu la kupata maarifa yatakayo badilisha mtindo wako wa ulaji ili uweze jenga afya bora.
Mahali na muda vitatangazwa hivi punde.
Kwa maeelezo zaidi piga simu 0673567890
SHARE.

KIWINajua wengi nikiuliza juu ya jina KIWI mtanitajia ile dawa ya kung'alishia viatu "Shoe Polish" inayotengenezwa na ka...
19/02/2020

KIWI

Najua wengi nikiuliza juu ya jina KIWI mtanitajia ile dawa ya kung'alishia viatu "Shoe Polish" inayotengenezwa na kampuni ya Johnson A Family.

Ukweli ni huu.

Kiwi ni aina ndege "bird" ambae anapatika nchini New Zealand.
Ndege huyu ni " National Symbol of New Zealand ", pia la jina ndege huyu ni jina la utani la watu wa New Zealand.

Mapema mwaka 1904 Wachina waliligundua tunda moja jamii ya "Berries" wakaliita Chinese Gooseberry.

Katika mwaka 1962, wakulima wa matunda nchini New Zealand wakaanza kulima matunda haya ya Gooseberry, ila wao tunda hili hawakuliita Chinese Gooseberry.

Waliliita KIWIFRUIT.

Unajua kwanini waliita hivyo, ni kuwa tunda hili la Chinese Gooseberry kimuonekano limefanana sana na ndege Kiwi, hivyo wakulima wa matunda nchini New Zealand wakaona bora waliite ivyo.

Mpaka leo tunda hili uitwa KIWI FRUIT.

( Tanzania matunda upatikana katika supermarket's)

DORIANI/DURIANAlama ya 🚭 "Hakuna kuvuta sigara" ni ujulikana sana katika maeneo ya umma, mashuleni,hospitalini,sheli,mao...
17/02/2020

DORIANI/DURIAN

Alama ya 🚭 "Hakuna kuvuta sigara" ni ujulikana sana katika maeneo ya umma, mashuleni,hospitalini,sheli,maofisini n.k.

Au alama ya 📵 "Simu haziruhusiwi" ni miongoni mwa alama zinazojulikana sana. Lengo la makatazo haya ni kuepusha hatari/majanga yanayo weza jitokeza kwa sababu za uvutaji sigara n.k.

Nchini Thailand,Japan,Singapore na Hong Kong, tunda la DURIAN limepigwa marufuku, mtu ukikutwa na tunda hili katika maeneo ya usafiri wa umma ( vituo vya mabasi,treni na viwanja vya ndege) unapigwa faini.

Na sababu ya kupigwa marufuku ni harufu mbaya ya tunda hili. Maji taka jumlisha mayai viza, mchanganyiko wa hivi ndio harufu ya durian, ila ajabu tunda hili ni lina faida nzuri kiafya, pia ni tamu sana.

Tanzania tunda hili upatikana visiwani Zanzibar kwa jina la DORIANI.

Bwana Matunda
Afyafruits Academy
+255 ( 0 ) 768839900 (WhatsApp)
©2020

Bwana MatundaMtaalam wa maswala ya lishe Mastidia Dionis February 05, 2020, katika ukurasa wake wa Facebook aliuliza swa...
16/02/2020

Bwana Matunda

Mtaalam wa maswala ya lishe Mastidia Dionis February 05, 2020, katika ukurasa wake wa Facebook aliuliza swali " TUNDA GANI UNALIPENDA SANA?". Jumla ya watu 19, waliweza kujibu swali hilo, kati yao watu (12) walisema tunda la Parachichi ndio tunda pendwa kwao. Watu (4) walisema tunda la Tikitimaji ni pendwa kwao, watu (2) walisema Nanasi, na mtu (1) alisema tunda lake pendwa ni Ndizi.
Majibu ya watu (19), yalitosha kueleza ni aina gani ya matunda yanayopendwa sana kuliwa nchini Tanzania, kuwa ni Parachichi,Nanasi,Tikitimaji na Ndizi, ukiachana na tunda la Nyanya ambalo kila siku watu ulitumia katika mapishi majumbani au mahotelini.
Tanzania ni moja ya nchi iliyo barikiwa ardhi yenye kustawisha matunda mbalimbali, kuanzia Parachichi,embe,chungwa,ndimu,limao,nanasi,ndizi,zabibu,tikitimaji,papai,fenesi,strawberry,mulberry,respberry,blueberry,blackberry,pera,fyulisi,apple,tango,komamanga,passion fruit,peazi,stafeli,nyanya,pilipili mboga na matunda mengi ya asili.
95% ya walaji wa matunda nchi Tanzania ula matunda kwa sababu ya ladha/utamu wa matunda. Kwa matunda ambayo sio matamu walaji ula kwa sababu ya desturi waliojiwekea mfano,tunda la Parachichi, walaji wengi ula tunda hili pamoja na wali au ugali sababu ya combination ya tunda ilo na milo hiyo. kula Parachichi pekee bila vyakula hivyo hawezi.
Matunda yenye sukari yamekuwa yakipewa nafasi kubwa sana katika jamii, na sababu kuu ni utamu wa matunda sio kingine.
Matunda k**a Tango,strawberry,limao,ndimu,fyulisi yamekuwa hayaliwi sana sababu hayana ladha au sukari, jamii imekuwa ikila matunda sio kwa sababu ya faida za kiafya zilizopo katika matunda. Jamii haijui faida za matunda yote, kuanzia yale yenye sukari na ya sio kuwa na sukari, kwa sababu hiyo ndio maana jamii uchagua yale matamu tu bila kujua ata yasio matamu yanafaida katika afya zao.
Matunda ni miongoni mwa vyakula vilivyo sheheni virutubisho muhimu vinavyoitajika mwilini kila siku. Mwili wa binadamu hauwezi fanya kazi, bila kupata virutubisho, ngoja nikuulize 'umewai kuona wapi gari linaendeshwa bila mafuta?', ndivyo mwili wa binadamu ulivyo.
Matunda ni chanzo kizuri cha virutubisho ivyo. Na matunda hayo ni yote yasio na ladha mpaka yale yenye utamu/sukari. Kila tunda lina aina ya pekee ya virutubisho na sio matunda yote yana aina moja ya virutubisho, ivyo ulaji wa matunda mchanganyiko ni bora na muhimu kiafya.
Virutubisho ni k**a Vitamini,Madini na Nyuzinyuzi.

TFSYL-Nikiwa na furaha na amani tele moyoni,ndani ya kijiji cha ITULAHUMBA-katika wilaya ya Mwanging'ombe, Mkoani Njombe...
15/02/2020

TFSYL-Nikiwa na furaha na amani tele moyoni,ndani ya kijiji cha ITULAHUMBA-katika wilaya ya Mwanging'ombe, Mkoani Njombe. Chini ya mti ambao unazalisha hewa safi na salama katika sayari ya tatu, uku ubaridi ukiwa nausikia kwa mbali, sababu ni mja nimevaa koti langu la babu nililoachiwa hulisi.
Nilipokaa pembeni yangu kuna bakuri,ndani ya bakuri kuna kisu na matunda mawili, matunda ambayo katika maduka ya vyakula pale Uingereza "OCADO" na "MAITROSE" matunda haya watu uyagombania kununua kila uchao.
Unajiuliza ni matunda gani hayo? ni haya ambayo ata yakae mwaka juu ya mti hayawezi kuiva kamwe,ndio ukiona nasema uongo pada mti wa matunda haya subiri ndani ya miezi 18-24 uamini nachosema. KIna Isaac Newton na wanasayansi wenzake matunda haya uyaita "Persea Americana".
Mkazi wa Oaxaca akikukuta una kula ovyo ovyo matunda haya anaweza kukuchapa ata kofi,ndio sababu matunda haya nchini kwao ni Nembo ya Taifa, najua unataka kujua ni nchi gani hiyo ni MEXICO.
Kipindi nataka kuanza kijimwambafai na matunda yangu, nikaanza kwanza kuyaosha taratibu, maana usalama ni jambo muhimu sana,kula bila kuosha matunda sio salama kiafya. Baada ya hapo kinyonge nikachukua kisu changu, na kuligawanisha tunda moja vipande idadi ya pembe kuu za dunia. Kipindi naendelea kula taratibu vipande vya tunda nililolikata,macho yangu kwa mbali sana yanamuona ndugu yangu Sanga anakuja, usiniulize kuwa siku hizi nimekuwa ndege Tai nawezaje kuona mbali sana, ukweli ni kwamba matunda haya yana faida moja kiafya "yanauwezo wa kuimarisha uwezo wa macho kuona vizuri".
Bwana sanga alipokuja akashangaa sana inawezekana vipi nakula matunda haya bila sahani ya wali pembeni, nikaangua kicheko cha mwaka, na kumwambia "kula matunda pamoja na milo mikubwa au baada ya kula mlo mkubwa k**a wali,huwezi ziona kuzipata faida za matunda kiafya ndugu yangu Sanga".
Basi tukaendelea na salamu na stori za kule na kule. Bwana sanga alisema 'hawezi kukaa sana kuna kilicho mleta asubuhi kwangu, bila kupoteza sekunde ni kuwa mke nyumbani k**a mbogo k**a sio nyati, ashikiki kawa mkali'. Nikahamaki nini tatizo?, Bwana Sanga akaendelea kusema "tatizo nini mimi (yeye)", nikasema "ati nini, umeshikwa ugoni Sanga?", akasema hapana bali siku hizi ushirikiano katika kujenga nyumba kwa mkewe umekuwa hafifu sana, yani sio mtungi tena bali jogoo hapandi mlima kufika kilele.
Nikatikisa kichwa ishara ya kusikitika kwa niliyo yasikia, maana najua nyumba bila ushirikiano sio nyumba, ndipo nikamwambia tiba ya tatizo lako ipo, ila kabla sijakupa nataka upande juu ya huu mti wa matunda tunayokula nidondoshe yote yaliokomaa vyema, Bwana Sanga anacheka na kusema "kwaio unanipa na adhabu", nikasema 'hapana' we pamba ukiyachuma yote chukua nenda nayo nyumbani, kayahifadhi sehemu salama ili yaive na ule maana hiyo ndio tiba ya tatizo lako, akashtuka "ebo ati nini? mimi nimekuja hapa sio kiutani utani, kivipi wewe unaniletea utani?".
Akapanda mtini na alipo maliza kuyachuma yote yalio komaa, niliagana nae akaanza safari ya kwenda kwake uku mimi nikiendelea kula vipande vyangu vilivyo bakia.
Miaka mitatu sasa, sijaonana na ndugu yangu Sanga tangu siku ile ya mwisho alipo kuja kuomba ushauri,sababu ni kuwa mimi niliama kijijini muda mrefu sana,ila bahati nzuri ni kuwa tunawasiliana na ananipa taarifa za familia yake, kuwa sasa ana watoto wawili, wenye afya bora sababu matunda niliyo mpa siku ile alihifadhi mbegu na kisha kuzipanda, na leo ana mashamba ya matunda yale niliyo mpatia. watoto wake wana uzito sawia sio nyama uzembe, wana akili sana sababu matunda wanayokula yana madini na viritubishi muhimu katika kujenga afya bora.
PARACHICHI/AVOCADO

HAPPY VALENTINE'S DAY
14/02/2020

HAPPY VALENTINE'S DAY

  Je umeshawai kupatwa na miwasho katika ulimi au mdomoni baada tu ya kumaliza kula Nanasi.K**a ndio fahamu ulikula Nana...
13/02/2020

Je umeshawai kupatwa na miwasho katika ulimi au mdomoni baada tu ya kumaliza kula Nanasi.

K**a ndio fahamu ulikula Nanasi lisiloiva vizuri, au halija menywa vyema au ulikula kiasi kikubwa cha nanasi.

13/02/2020

Address

Songea
Songea

Telephone

+255622504949

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Fruits posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Afya Fruits:

Share