Cheka Nasi. Pata Mpya Za Leo

Cheka Nasi. Pata Mpya Za Leo Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Cheka Nasi. Pata Mpya Za Leo, Grocers, Kabare, Muleba.

Wapendwa kheri ya Mwaka mpya 2025....
01/01/2025

Wapendwa kheri ya Mwaka mpya 2025....

WASANII MOTOMOTO
24/12/2024

WASANII MOTOMOTO

23/12/2024
22/12/2024

HI MEMBERS.... NISEME NISISEME?

JAMANI, KITU RAHISI UNACHOWEZA KULAZIMISHA KIWE CHAKO NI MAFANIKIO YAKO TU. NA SIYO MOYO WA MTU.
MI NAPITA TUU JAMANI...

MTAJE ULIYEMJUA HAPO
22/12/2024

MTAJE ULIYEMJUA HAPO

Kila mtu hubeba mzigo wake tofauti ni kwamba mzigo umebebea wapi?
22/12/2024

Kila mtu hubeba mzigo wake tofauti ni kwamba mzigo umebebea wapi?

Bashungwa aanza na moto... Vitambulisho
17/12/2024

Bashungwa aanza na moto... Vitambulisho

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhakikisha vitambulisho milioni moja na laki mbili ambavyo tayari vimeshatengenezwa vinasambazwa na kuwafikia wananchi walengwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Desemba 17, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.

"Ni wajibu wenu (NIDA) kuhakikisha kadi hizi mnazifutilia na zinawafikia walengwa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, nitakaporudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa" amesema Bashungwa

Waziri Bashungwa ameiagiza NIDA kuhakikisha inatengeneza vitambulisho vipya bila gharama yoyote wala usumbufu kwa baadhi ya Watanzania ambao Vitambulisho vyao vilifutika maandishi kutokana na tatizo lililotokea katika uzalishaji.

Aidha, Bashungwa ameitaka NIDA kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuondoka na tabia ya urasimu ambapo ameiagiza menejimenti kuanza kuwachukuliwa hatua baadhi ya watumishi wazembe ambao hawatoi huduma nzuri kwa Watanzania.

17/12/2024

Mkazi wa Nkalalo wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Nicholaus James (21), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne (jina linahifadhiwa) wa sekondari ya Taro wilayani humo.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 22882/2024, James ametiwa hatiani na Mahakama ya wilaya Kwimba kwa kosa la kumbaka binti ambaye utambulisho wake unahifadhiwa kwa sababu za kisheria (19) mwanafunzi wa kidato cha 4 shule ya sekondari Taro.

Awali, Mwendesha Mashtaka aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 07.08.2024, katika Kijiji cha Nkalalo, wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza kinyume na vifungu vya 130(1)(2)(a) pamoja na kifungu cha 131(1) cha Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya sheria marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 14.08.2024 na kusomewa shtaka hilo ambalo alilikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe 21.08.2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Baada ya Mahakama kusikiliza mashahidi watano (5) wa Jamhuri akiwemo Mganga aliyemfanyia uchunguzi binti huyo, Mahakama ilijiridhisha bila ya kuacha shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Aidha, Mahakama hiyo ilielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa kumvizia binti huyo wakati amekwenda kuchota maji na kumkamata kwa nguvu kwa kumtishia kumchoma kwa kisu na kisha kumchania nguo zake za ndani.

Baada ya kutiwa hatiani mshtakiwa aliiomba Mahakama imuachilie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza kakini Mwendesha Mashtaka aliisisitiza Mahakama kumpa adhabu kali mshtakiwa kwa sababu watu wa namna yake ni hatari kwenye jamii na wamekuwa wakididimiza na kukatiza maendeleo ya wabinti wenye ndoto za mafanikio.

Licha ya shufaa hizo za mshtakiwa, Hakimu Jagadi alimuhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

17/12/2024

🔰𝐍𝐄𝐗𝐓 𝐌𝐀𝐓𝐂𝐇🔰

🏆
⚽️ Young Africans SC🆚Mashujaa FC
📆 19.12.2024
🏟 KMC Complex
🕖 10:00 Jioni


Address

Kabare
Muleba
POSTCODE

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Cheka Nasi. Pata Mpya Za Leo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Cheka Nasi. Pata Mpya Za Leo:

Share

Category