Ustawi wa jamii.comdv

Ustawi wa jamii.comdv Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ustawi wa jamii.comdv, Grocers, 584, Korogwe.

04/11/2024

upendo ni nini ????

Upendo ni tendo lolote linalomwezesha mtu kutabasamu iwe asubuhi, mchana, jioni au usiku

Kutabasamu ni ishara ya furaha

Furaha huambatana na amani

Kutabasamu huonekana usoni na inajulikana kwamba "the face is the index of the heart"

Kila mmoja wetu anahitaji kutendewa mema ili aweze kutabasamu.

Wataalamu wa afya wamethibitisha kuwa furaha na tabasamu "is the natural healing of numerous health consequences"

Leo umewasababishia watu wangapi tabasamu?

Katika mwenendo wako unawaondolea au unawaongezea watu tabasamu?

Wewe mzazi
Wewe mtoto
Wewe kiongozi
Wewe mtumishi

Nafasi yako ni ipi katika somo la leo

01/11/2024

Unatakiwa ucheke kidogo sio sana ndio kidonda kitapona mapema

Hutakiwi kukasirika ndo kidonda kitapona mapema

Upate supu ya mifupa ndo kidonda kitapona

Upumzike vizuri ndo kidonda kitapona mapema

Usiwe na msongo wa mawazo ndo kidonda kitapona

Usikumbuke mambo yalokuumiza ndo kidonda kitapona mapema

Upate maziwa fresh yachemshwe na kukorogea vijiko viwili vya asali ndo kidonda kitapona mapema

Upate mboga za majani fresh hasa mchicha yaoahwe vizuri na kuchemshwa itoe supu sio kukaanga, ndio kidonda kitapona mapema

Ukae na kupiga zoga na mtu au watu wanaokupenda ndo kidonda kitapona mapema.

Uwapende wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kinyongo ndio kidonda kitapona mapema.

Kusali na kujiamimi ndio kidonda kitapona mapema

Usafi wa mwili, mavazi na kitanda ndo kidonda kitapona mapema

Ufanye mazoezi ya kutembea kwa maelekezo ya mtaalamu wa afya ndo kidonda kitapona mapema

31/10/2024

Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa waziri wa Tamisemi.

Watumishi wanaofanya kazi katika maeneo ya vijijini ni k**a wamekatiwa Bima ya NHIF bure.

Nasema bure kwasababu zifuatazo:

Mosi
Vijiji vingine Tanzania Bara havina zahanati zinazotumia Bima

Pili
Unaweza kwenda zahanati au kituo cha afya au hospital ukakosa dawa inayoendana na tatizo lako. Hivyo unalazimika kwenda kununua kwenye pharmacy wakati wizara ya afya na NHIF inakata hela kila mwezi ya kutuhudumia

Tunaomba mtuangalie katika hilo

22/09/2024

Hello sir.

Long time we didn't make conversation.

Tofauti mojawapo kati ya taasisi za umma na NGOs ni taasisi za umma mathalan shule za serikali kuwa ni taasisi za matokeo bila programming.

Hata privates wanataka matokeo pia.

Tofauti inatokea pale taasisi za umma zinamtaka mwalimu mkuu alete matokeo mazuri bila programming.

Hapa programming namaanisha strategies/plans, investment and implementations of programs.

Both institutes wanafanya programming lakini hutofautiana kwenye investment and implementations of programs.

Ninaposema investment nimaanisha kuwekeza katika utekelezaji wa mikakati.

Uwekezaji wowote ule unahitaji raslimali au mtaji.

Mtaji au raslimali hugawanyika katika sehemu kuu mbili ambayo ni raslimali watu na raslimali vitu.

Raslimali vitu hujumuisha equipped and conducive environment for teachers to teach and pupils to learn.

Katika eneo hili taasisi nyingi za umma have neither equipped nor conducive environment to facilitate teaching and learning.

Katika eneo la raslimali watu taasisi nyingi za umma hazina walimu wa kutosha kuweza kuleta matokeo halisi.

Binafsi sielewi hii changamoto ya raslimali watu inaanzia wapi!

21/09/2024

Wasanii Wote Tanzania Na Afrika Tungeni Nyimbo Za Ukombozi Kamili Wa Afrika.

Kuanzia Sasa Wasanii Elekezeni Kazi Zenu Kwa Ukombozi Kamili Wa Mwafrika.

Waangalizi Wa Taasisi Za Dini Elekezeni Hutuba Zenu Katika Ukombozi Kamili Wa Mtoto Wa Afrika.

Wanazuoni Na Vyuo Vikuu Vyote Unganeni Na Pan-Africanist Kupigania Uhuru Kamili Wa Bara Letu.

Bidii Yoyote Mtakayofanya Kuipatia Afrika Uhuru Kamili Ni Matunda Ya Vzazi Vijavyo Kwan Nasi Tunainjoi Matokeo Ya Bidii Ya Vizazi Vizazi VilivyopitĂ  k**a vile KWAMME NKRUMAH, PLO, MWL J. K. NYERERE, NELSON MANDELA ETC.

01/08/2024

Hakuna mwalimu mwenyewe maslahi na Cwt

Wenye maslahi na chama hichi ni ile safu ya uongozi tu.

Walimu wengine wote wanakula kwa macho tu.

Imagine

Watu wamejiteua, wamejichagua, wamejiajiri na wameajiri kwa pesa za majasho ya watu wengine.

Hawana huruma kabisa.

Hii dalili sio njema.

Ni dalili za kuendelea kumkandamiza mwalimu na kumfanya mnyonge kabisa.

Na kwa bahati mbaya walimu wengi ni waoga.

Wengi wetu ni kina ndio mzee.

Sasa hapo hakuna usalama kabisa

01/08/2024

Imagine
Fedha zinakusanywa na Cwt halieleweki ni kwaajili gani!

Imagine
Sisi sisi watoto wa KALAMBWANDILA hatujui k**a Cwt imewahi kuanzisha miradi ya kiuchumi!

Imagine
Cwt ina mwenyekiti

Cwt ina katibu

Cwt ina katibu mkuu

Cwt ina Rais

Cwt ina naibu katibu

Imagine nani anawalipa hao viongozi?
Au wanajilipa na hiyo fedha zetu?
Huyo Rais, mwenyekiti, katibu, katibu mkuu na naibu katibu anatufanyia nini mpaka alipwe kwa hela zetu?

Hivi tume haitoshi kutetea maslahi ya mwalimu?

Imagine
Jaribu kufikiria k**a mwalimu wa Kata ya Kizara anafaidika nini na Cwt? Just thinking about this number of people who are waiting to collaborate on your little salary.

Rais

Makamu Rais

Katibu mkuu

Katibu
Naibu katibu

Mweka hazina
Mjumbe kutoka kila mkoa

Mwakilishi walimu walemavu

Mwakilishi walimu vijana.

Bora tu warudi kufanya kazi waliosomea kuliko kusubiri kukamua jasho alilovuja mtu mwingine.

Mwenyezi Mungu ametuagiza tule jasho la mikono yetu.

19/07/2024

Amka kumekuuucha!

Wanasiasa ni wanafiki lakini hawajafikia watu wa dini yako.

Imeandikwa pendaneni ninyi kwa ninyi na hii ndio amri kuu kuliko yote

Katika suala la ustawi kiuchumi Africa inazidi kurudi nyuma, niulize kwanini.

Hata suala la kikokotoo mheshimiwa Rais hakuelezwa kikamilifu.

Bunge la chama kimoja ni sawa na nyumba inayoshikiliwa na nguzo moja.

Too much monotonous is harmful, yaani huwezi kulalia ubavu mmoja usiku kuchere ama sivyo you are dead.

Bongoland na Africa ina viongozi wanaotaka matokeo bila mikakati, uwekezaji na utekelezaji

Ukila na kipofu usimshike mkono, yaani ukimwamusha alalaye utalala wewe.

Ganzi iliyompata panzi imemleta kunguru furaha.

Ujinga wako ndio ushindi wao

West or East home is the best

13/07/2024

Sijui ni lini bara letu la Africa itapata nguvu like Europe, America and Asia and also posses total defense as well as other continents.

Just imagine what the African children are taught in schools, churches, mosques and other gatherings.

79% of religious teachings which African children receive is self hate education.

Till this time I don't know what Africans need.

Imagine!

Very sorry if I upset you

Katika miondoko ya zouk na miziki yote ya zamaniHakuna collision Hakuna kupakatana Hakuna kupambana Hakuna kutimbana Kil...
13/07/2024

Katika miondoko ya zouk na miziki yote ya zamani
Hakuna collision
Hakuna kupakatana
Hakuna kupambana
Hakuna kutimbana

Kila mtu anacheza kifyake kwa uhuru huku akiashiria approaching the opposite s*x without touching him or her

Una maoni gani?

31/05/2024

Tanganyika, Zanzibar na muungano.

Ni sawa na wanawake wawili na mwanamme mmoja.

Mke wa kwa kwanza ni Tanganyika

Mwanamke wa pili ni Zanzibar

Mwanamme ni muungano.

Mwanamke wa kwanza tuseme Tanganyika ana watoto lakini umemfukuza, hutaki awalelee watoto wake.

Mwanamke wa pili tuseme Zanzibar unampenda na unawapenda na watoto wake.

Wewe muungano huoni unawanynyasa watoto wa Tanganyika?

Mpe yao ruhusa akae nao ili akusaidie kulelea familia yako.

SoMo
Tunaomba katiba iliyopendekezwa na tume ya jaji Warioba.

Address

584
Korogwe

Telephone

+255786401446

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ustawi wa jamii.comdv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category