27/08/2024
... π π‘ππ¦ππππππππ‘π
Nimeona mijadala kuhusu kampuni ya (GSM) kudhamini zaidi ya timu moja ligi kuu. K**a mnijuavyo huwa napenda kufanya tafiti na kuja na FACTS zenye ushahidi.
βΉοΈ Katika utafiti wangu mdogo nimegundua kuna Makampuni zaidi ya manne yanadhamini zaidi ya timu moja ligi kuu Tanzania bara huku wengi macho wakiyaelekeza kwa (GSM) pekee.
Nimebaini wengi hawajui kuwa endapo Bodi ya ligi ikiamua kubadili kanuni kutoruhusu kampuni moja kudhamini zaidi ya timu moja kuna timu ndogo nyingi ZITAATHIRIKA na kuwaacha Simba na Yanga wakiendea kutamba MILELE na MILELE.
Kampuni zinazodhamini timu zaidi ya moja ligi kuu Tanzania bara 24|25
β Azam TV - 16
β TBC - 16
β GSM - (6)
PM-BET
β Pamba Jiji.
β Ken Gold.
β Tanzania Prisons.
β Dodoma Jiji.
β Singida Black Stars
Elsewedy cables
β Dodoma Jiji
β Tanzania Prisons,
β KMC Football Club.
β Coastal union.
β JKT Tanzania
Azam Max
β Namungo FC
β Azam FC
Sportpesa
β Young Africans SC
β Fountain Gate
etc.......
Kanuni ya kuzuia udhamini ambayo haipo ikitungwa haitamuathiri (GSM) itakwenda kuviathiri vilabu vidogo.
Nanukuu :
βHakuna kanuni inayozuia mdhamini mmoja kudhamini zaidi ya timu moja. Udhamini ni jambo la kikanuni, madhumuni ya kanuni kwa asilimia 90 yameelekezwa kwenye klabu husika, timu, wachezaji, waamuzi, viongozi, mbali na mijadala iliyoibuka kuhusu (GSM) hakuna klabu yoyote au mdau kuelekea msimu huu aliyelalamikia suala hilo"
βLakini mimi siku zote nimekuwa nikiamini kuwa kanuni siyo msahafu, zinajadilika, zinabadilishika kwa hiyo pale ambapo wadau wataona kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kanuni k**a ambavyo siku zote tumekuwa tukifanya basi milango ipo wazi"
"Kanuni hupitishwa na vilabu vyote vya ligi kuuu lakini mpaka sasa hakuna klabu iliyokuja kulalamika kuhusu suala hilo, tunasikia tu mitandaoni"
Β©οΈ Almas Kasongo
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi.
βΉοΈ Tunapojitahidi kuhimiza kanuni itungwe kuzuia udhamini wa timu zaidi ya moja kwa ksmpuni moja tukumbuke kuna zaidi ya kampuni nne sio (GSM) pekee ambazo zikijitoa zile kelele za timu ndogo kushindwa kusafiri zitarejea tena k**a zamani wakati ambao tulikuwa tukililia makampuni yaje kwenye soccer kuwekeza.
βΉοΈ Kwa mujibu wa (FIFA), hairuhusiwi mtu au kampuni moja KUMILIKI timu zaidi ya moja kwenye ligi moja. (FIFA) haizuii 'SPONSORSHIP' UDHAMINI kitu ambacho wanakifanya GSM, PM-BET, AZAM TV, TBC, MELIDIAN BET, AZAM MAX, SPORTPESA, M-BET, ELSEWEDY CABLES na makampuni mengine kwenye ligi yetu.