15/01/2024
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
CHIDI MPISHI HAPA NAKUFUNZA KUPIKA VITUMBUA
Kuna aina nyingi ya utengenezaji wa vitumbua. Leo napenda tujifunze aina hii;
*Mahitaji*
🌹Mchele kilo 1
🌹Sukari 1/4kg
🌹Tui la n**i 3/4
🌹Hiliki ya unga 2tbs
🌹Hamira 2tbs
🌹Mafuta ya kupikia
🌹Unga wa mahindi 6 tbs
🌹Unga wa ngano 3 tbs.
*Matengenezo*
*K**a unatumila blenda*
🌹Loweka mchele wako masaa 6-12 na toa kwenye maji.
🌹🌹Weka kwenye blenda na saga kidogo, kisha ongeza weka hamira, hiliki na tui lako la n**i kisha saga tena,,,, mchele wako ukilainika weka Sukari na saga tena mpaka ule mchanganyiko wako ulainike,,,, baada ya hapo weka unga wa mahindi na saga kidogo kisha ongeza unga wa ngano na saga tena ili ichanganyike vizuri. Baada ya hapo weka kwenye container au bakuli na funika kwa 30dk - lisaa 1.
🌹🌹🌹 Anza kuchoma k**a ifuatavyo,,,,, weka chuma chako jikoni na acha kipate moto. Weka mafuta nusu kijiko katika kila chumba cha chuma chako,,,, Tumia upawa kuchotea na mimina kwa kila chumba. Acha kwa dk 3 na geuza upande mwingine,,,, weka tena mafuta nusu kijiko na acha kwa dk 3 tena,,,,, kitumbua chako kitakuwa tayar,,, geuza kila upande na ukiona kimekua na rangi ya udhurungi ya kupendeza kutambua chako kitakuwa tayar,,,, fanya hivyo kwa vitumbua vyote.
Hakikisha moto ni wa wastani ili usiunguze wala kubabua kitumbua chako.
*K**a hauna blenda*
Loweka mchele wako kwa masaa 3-6 na toa kisha tandaza vizuri ili ukauke
Maji yakikauka peleka kwa mashine na usage.
Weka kwa unga wa mchele kwenye bakuli kisha weka Sukari, hiliki, hamira na n**i kisha koroga vizuri mpaka ichanganyike vizuri ongeza unga wa mahindi na koroga tena kisha ongeza unga wa ngano na koroga tena.
Baada ya hapo anza kuchoma k**a nilivyoelekeza hapo juu.
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
Ukipenda waweza weka mayai 3 kwa huo mchanganyiko wako.
Tumia stick au kijiti kilichochongwa vizuri kugeuza vitumbua vyako,,,, pia waweza tumia spo