Bongo Dar es salaam

Bongo Dar es salaam Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Bongo Dar es salaam, Grocers, ARUSHA, Arusha.

17/08/2023

Mfumo wa exhaust(Mfumo wa kutolea uchafu nje).

14/08/2023

FAHAMU JINSI YA KUSOMA MATAIRI

Ulishawai kuangalia pembeni mwa tairi na kukuta kuna herufi na namba na ukatamani kujua nini maana yake. Nimewaletea ishara na alama ambazo huwekwa kwenye tairi ili kila dereva ajue nini maana zake.

Alama ambazo huwekwa kwenye tairi huelezea;

1. Ukubwa wa tairi.
Baadhi huwekewa maeleze kuhusu ukubwa wa tairi na ni maelezo muhimu sana kuwepo kwenye tairi. Kila namba na kipengele inakua na maana tofautitofauti kwenye tairi. Inaonekana k**a hivi;
165/65/R14 79 T.

• 165 - Upana wa tairi kwa milimita

• 65 - Urefu wa tairi kutoka chini kwenda juu kwa asili demia. Mfano, ni asilimia 65 ya upana wa tairi.

• R - inamaanisha kipenyo cha tairi yaani Radius kwa lugha ya wenzetu

• 14 - Inamaanisha ukubwa wa rim kwa kipimo cha inchi.

• 90 - 90 code ya uzito wa kubeba

• V - Inamaanisha speed/Kasi.

Herufi “V” yenyewe ipo hapa kwa mfano na inaweza ikawa herufi yeyote k**a vile “H”, “L”, “M”, “N” “O” “P” “Q” “R” “S” “T” “U” “V” “W” “Y”“W”.
Herufi hizi zinawakilisha mwendo kasi unaoruhusiwa na matairi haya. Na ili uweze kuzielewa zipo indices ambazo zinatambulika kimataifa k**a tafsiri sahihi ya mafumbo-namba haya.

Mafumbo ya mzigo kiasi gani unaruhusiwa kwa tairi yako;
62…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 265
75…… inaruhusiwa kubeba hadi Kg 387
88…….inaruhusiwa kubeba hadi Kg 560
101…...inaruhusiwa kubeba hadi Kg 825
114……inaruhusiwa kubeba hadi Kg 1180
63….....inaruhusiwa kubeba hadi Kg 272
76….....inaruhusiwa kubeba hadi Kg 400
89….....inaruhusiwa kubeba hadi Kg 580
102…...inaruhusiwa kubeba hadi Kg 850
115…...inaruhusiwa kubeba hadi Kg 1215
64…….inaruhusiwa kubeba hadi Kg 280
77…….inaruhusiwa kubeba hadi Kg 412
90…….inaruhusiwa kubeba hadi Kg 600
103…...inaruhusiwa kubeba hadi Kg 875

Hivyo k**a gari yako ina namba 62 ambayo inaruhusu kubeba hadi 265Kg tu huwezi kubeba mzigo wenye uzito wa 600Kg ambao tairi yenye nambari 90 ndiyo inayomudu au yenye nambari ya juu Zaidi.

Mafumbo namba ya mwendo kasi na maana yake ni k**a yafuatayo:
L…..inaruhusu hadi 120 Km/h.
M…..inaruhusu hadi 130 Km/h
N…..inaruhusu hadi 140 Km/h
P…..inaruhusu hadi 150 Km/h
Q…..inaruhusu hadi 160 Km/h
R…..inaruhusu hadi 170 Km/h
S…..inaruhusu hadi 180 Km/h
T…..inaruhusu hadi 190 Km/h
U…..inaruhusu hadi 200 Km/h
H…..inaruhusu hadi 210 Km/h
V…..inaruhusu hadi 240 Km/h
W…..inaruhusu hadi 270 Km/h
Y…..inaruhusu hadi 300 Km/h

Hivyo ikiwa tairi yako ina namba L inayokuruhusu spidi hadi 120 na si Zaidi, jua hauwezi kuendesha kwa spidi 150 ambayo ni kwa ajili ya nambari “P” au ya Zaidi yake.

2. Kuonesha uelekeo.
Sio matairi yote huonesha uelekeo, ni muhimu kujua ni sehemu gani au upende gani wa tairi unatakiwa kuzunguka. Yaana namaanisha ni upende gani utakiwa kukaa nje na upende gani kukaa ndani. Pia Kuna matairi huwekwa direction ya tairi kuzungukia.

3. Kiwango kikubwa cha mizigo na shinikizo.
Matairi yana kiwango cha mwisho cha kubeba mizigo pamoja na shinikizo(pressure). Kitabu chako kitakuonesha ni kiwango gari inatakiwa ibebe ambayo ni sahihi kwa uendeshaji wako wa kilasiku.

4. Kiashiria cha tairi kuisha.
Baadhi ya watengenezaji wa matairi huweka kikomo cha kukanyaga au kuisha kwa matairi. Kikomo hichi kimewekwa pindi tairi lako likiisha na kufikia 1.6 milimita unahitaji kubadilisha tairi. Hapa kibongobongo tunasema tairi linakipara.

Mengine ni k**a brand ya tairi, nchi lilipotengenezewa, material na pattern.

Pia matairi yanaelezea mwaka yalipotengenezwa.

Ukiangalia kwenye picha chini kuna namba nne za mwisho ambazo ni hizo 1309:
13 - inamaanisha wiki ya tairi kutengenezwa.
09 - inamaanisha mwaka wa kutengenezwa

Kwaio tairi limetengenezwa wiki ya 13 mwaka 2009.

Usisite kutufollow kwenye kurasa yetu Mycar Tanzania like, comment na share ili uwe wa kwanza kupata update.

14/08/2023

TAIRI KUPASUKA

JE UNAFAHAMU NINI CHA KUFANYA TAIRI LINAPOPASUKA WAKATI GARI INATEMBEA?

1. Usipanic wala usikanyage p**o ya breki kwani hii itapelekea gari kuyumbayumba barabarani. Unachotakiwa ni kwenda nalo ili uweze kulidhibiti gari.

2. Shika usukani vizuri na mikono yote miwili, usijaribu kukata kona, zingatia umakini wako barabarani na mwendo wa gari kwani mara nyingi gari hupoteza muelekeo tairi inapopasuka.

3. Endelea na mwendo uliopo ili gari iendelee kutembea na usiondoe mguu kwenye p**o ya mafuta hapo hapo (kwa gari ya Manual)

4. Ondoa mguu kwenye p**o ya mafuta taratibu (Usijaribu kukanyaga p**o ya breki kabisa), ukijaribu kukanyaga breki gari inaweza kupinduka. Mwendo wa gari utaendelea kupungua huku ukiendelea kuwa makini katika barabara.

5. Weka gia ya neutral huku unaendelea kuweka umakini barabarani

6. Mwendo wa gari ukipungua na kuwa chini ya 60kph, taratibu kanyaga breki huku ukijaribu kwenda pembezoni mwa barabara ili kusimama.

7. Hapa itakua salama kusimamisha gari yako na kuzima injini ili kulinda maisha ya abiria wako na wewe mwenyewe.

Usisite kutufollow kwenye kurasa yetu Mycar Tanzania like, comment na share ili uwe wa kwanza kupata update.

13/08/2023

TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE

1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.

2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.

3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:

(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali

(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri

(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara

4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.

5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).

6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.

7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT

8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya nyeupe

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.

9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza.

Soma na ufahamu tofauti za namba zinazowekwa kwenye magari.

Usisite kutufollow kwenye kurasa Mycar Tanzania like comment na share ili uwe wa kwanza kupata update.

11/08/2023
11/08/2023

Hakunaga Full Time 2 mechi iliisha nyau nyau ila ndo hivyo tu wachezaji wakabaki uwanjani utani utani nashangaa makolokwinyo wana shangilia tu

Anyway kwa kikosi hiki dakika ya 20 tu Yanga bingwa wa kombe la Ngao ya jamii ..

Na nyie azam tusubirini tunakuja mtatuambia tu

09/08/2023

Address

ARUSHA
Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo Dar es salaam posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category