Mbunge LAKI

Mbunge LAKI Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mbunge LAKI, Grocers, KWAHANI, Zanzibar.

22/05/2026

Nawatakia wananchi wangu wote wa Jimbo la Kwahani pamoja na waumini wote Ijumaa Mubarak yenye kheri, baraka na amani.

Mbunge wa Jimbo la Kwahani na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Mohamed Laki, akiwa ...
21/05/2026

Mbunge wa Jimbo la Kwahani na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Mohamed Laki, akiwa pamoja na wabunge wenzake wa k**ati hiyo walipokutana na nyota wa zamani wa soka wa Uingereza, Rio Ferdinand, jijini Dodoma.

Rio Ferdinand, ambaye aliwahi kung’ara katika klabu ya mashetani wekundu Manchester United pamoja na timu ya taifa ya Uingereza, alishiriki mazungumzo yaliyojikita katika maendeleo ya michezo, hususan soka, na nafasi yake katika kukuza vipaji na kuwajengea vijana fursa za maendeleo nchini.

Aidha, mkutano huo uliibua hamasa na mtazamo mpya kuhusu mchango wa michezo katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mh. Mohamed Laki ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani, ampongeza Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti ...
16/05/2026

Mh. Mohamed Laki ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani, ampongeza Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kutimiza ahadi yake kwa vijana, aliahidi wakati wa kampeni na sasa ametenda kwa vitendo, jambo linalodhihirisha kuwa ni kiongozi mtekelezaji mwenye uongozi unaoacha alama.

Hatua hiyo imeleta faraja na matumaini makubwa kwa vijana, huku ikionesha dhamira ya kweli ya Dk. Mwinyi katika kutekeleza yale aliyowaahidi wananchi wakati wa kampeni.

Hakika huu ni uongozi unaowacha alama.

15/05/2026

Ijumaa Kareem.

Mh. Mohamed Laki, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani na pia Rais wa Shirikisho la Sanaa Zanzibar, anatarajiwa kuwepo n...
14/05/2026

Mh. Mohamed Laki, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani na pia Rais wa Shirikisho la Sanaa Zanzibar, anatarajiwa kuwepo na kushiriki katika tukio maalum la “SHUKRAN BI MKUBWA” lililoandaliwa na Rukia’s Sweets.

🌟 Mgeni Rasmi: Mhe. Mama Mariam Mwinyi – Mke wa Rais wa Zanzibar

📅 Tarehe: 16 Mei 2026
🕗 Muda: Saa 1:00 Usiku
👔 Mavazi: Black / Light Blue
📍 Ukumbi: Sunshine Hall

TUNAKUENZI LEO, TUPO PAMOJA NAWE.

Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Mh. Mohamed Laki, amepongeza na kufurahishwa na kauli ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa B...
12/05/2026

Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Mh. Mohamed Laki, amepongeza na kufurahishwa na kauli ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuhusu mpango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa vibali vya ajira mpya kwa wauguzi pamoja na kada nyingine za afya katika bajeti ya mwaka 2026/2027, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. Akizungumza kauli hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.

Kwa hakika, vipaji na ubunifu vinahitaji kuthaminiwa, kuendelezwa na kutuzwa zaidi, kwani ni miongoni mwa ajira muhimu n...
12/05/2026

Kwa hakika, vipaji na ubunifu vinahitaji kuthaminiwa, kuendelezwa na kutuzwa zaidi, kwani ni miongoni mwa ajira muhimu na zinazokua kwa kasi duniani, huku zikiwapatia vijana na jamii kipato pamoja na fursa mbalimbali za maendeleo.

Katika kuonesha hali hiyo, kijana Sleiman Abdallah maarufu k**a (Nyenzo) amechora picha ya Mh. Mohamed Laki, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani, na kumkabidhi picha hiyo k**a ishara ya upendo, heshima na kuthibitisha kipaji chake cha kipekee katika sanaa ya uchoraji.

Hatua hiyo imeonesha namna sanaa inavyoweza kuwa daraja la kuibua vipaji, kuunganisha jamii na kuwapa vijana nafasi ya kujieleza pamoja na kujitafutia maendeleo kupitia ubunifu wao.

09/05/2026

Mh. Mohamed Laki ambae ni Rais wa shirikisho la sanaa Zanzibar, Pia ni mbunge wa Jimbo la Kwahani, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Msanii Zanzibar yaliyofanyika tarehe 05 Mei 2026 katika ukumbi wa Nyumba ya Sanaa Mwanakwerekwe, Zanzibar, ambapo aliwahimiza wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa sanaa kushirikiana kwa pamoja katika kuikuza na kuiendeleza sanaa ya Zanzibar.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Laki alisisitiza umuhimu wa mshik**ano, ubunifu na ushirikiano kati ya wasanii, wadau na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha sanaa inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Aidha, aliwataka wadau wa sanaa kuendelea kuwaunga mkono vijana wenye vipaji kwa kuwapatia fursa na mazingira bora yatakayowasaidia kufikia ndoto zao kupitia sanaa.

06/05/2026

Mh. Mohamed Laki, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kwahani, ametoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kufuatia hatua ya kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kutoka shilingi 300,000 hadi 500,000.

05/05/2026

Mh. Mohamed Laki, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Sanaa Zanzibar na pia Mbunge wa Jimbo la Kwahani, akizungumza na wasanii katika mkutano na waandishi wa habari (press conference) kwa kuadhimisha siku ya msanii Zanzibar uliofanyika leo katika ukumbi wa Nyumba ya Sanaa Mwanakwerekwe, Zanzibar.

Katika mazungumzo yake, Mh. Mohamed Laki aliwahimiza wasanii kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao, akibainisha kuwa wasanii wana uwezo wa kukopesheka na kujiinua kiuchumi kupitia kazi zao za sanaa. Aidha, alieleza matarajio yake kuwa maadhimisho ya Siku ya Msanii Zanzibar yawe endelevu kila mwaka na yawe na matokeo chanya yatakayochochea maendeleo ya tasnia ya sanaa.

Vilevile, alisisitiza umuhimu wa kila uongozi unaoongoza shirikisho hilo kuacha alama chanya kwa kuweka mikakati madhubuti itakayokuza na kuendeleza sanaa Zanzibar kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

#

Address

KWAHANI
Zanzibar
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbunge LAKI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category