20/03/2022
JE WAJUA UTOFAUTI ULIOPO KATIKA YA MISA TAKATIFU NA IBADA TAKATIFU?
• Kiukweli hili swali linawachanganya Waamini wengi hasa sisi tunaojiita Wafuasi wa Kristo, kila mmoja ukimuuliza hili swali, atakupa jibu tofauti kulingana na Imani yake.
• Hivyo basi napenda nitumie fursa hii kuelezea utofauti uliopo kati ya Misa Takatifu na Ibada Takatifu k**a ifuatavyo:-
• Kwa Wenzetu Wasabato, Walokole na Madhehebu mengine, wao hawana kitu kinachoitwa Misa Takatifu, bali wana Ibada Takatifu tu kila wanapokusanyika kwa lengo la kumwabudu Mungu.
• Lakini uzuri ulioje kwetu sisi Wakatoliki, tuna vyote hivi viwili kwa pamoja, na kila kimoja kinafanyika kwa wakati wake uliopangwa na Mama Kanisa.
Swali: Sasa je huo utofauti ni upi?
Jibu: ⬇️⬇️⬇️⬇️⬇️
1. IBADA TAKATIFU
➖Ni sehemu pekee katika Kanisa, ambayo kwa ujumla imebeba Liturjia moja tu, nayo ni Liturjia ya Neno.
➖Mara nyingi katika Ibada Takatifu, inaweza kuongozwa na yeyote yule, hasa mwenye kujua utaratibu mzuri wa kusalisha na kuwaongoza watu katika Maombi.
➖Ibada Takatifu inaweza kufanyika katika Misiba, Kushiriki Jumuiya, Kusali Rozali Takatifu, Kuabudu Ekaristi Takatifu, Kuabudu Msalaba siku ya Ijumaa kuu, Kupakwa Majivu na hata Sala zako binafsi pia nayo huitwa Ibada Takatifu.
2. MISA TAKATIFU
➖Ni kilele na kikomo cha Ibada zote unazozijua wewe duniani, katika Misa tunaunganika moja kwa moja na Kristu.
➖Hivyo utofauti uliopo ni kwamba, Misa Takatifu ina Liturjia mbili, ambazo ni Liturjia ya Neno na Liturjia ya Ekaristi Takatifu.
➖Mara nyingi Misa Takatifu haiwezi kuongozwa na kila mtu, bali ni kwa yule aliyepewa Daraja Takatifu tu yaani Mapadre, Maskofu au Baba Mtakatifu.
➖Misa ili iitwe Misa Takatifu, inapaswa kuwepo na vitu viwili, navyo ni Mkate na Divai. K**a hakuna hivi vitu, basi hiyo sio Misa Takatifu bali itaitwa Ibada Takatifu.
• Mwisho napenda kuhitimisha kwa kusema kuwa, kuna desturi ya Waamini ukiwauliza unaenda wapi? Atakujibu naenda Kanisani, hapana sema "Naenda kwenye Ibada Takatifu au kwenye Adhimisho la Misa Takatifu" na sio "Naenda kwenye Ibada" k**a wengi tulivyozoea.
TUMSIFU YESU KRISTO..
www.radiombiu.co.tz