Ukerewe MINI Market

  • Home
  • Ukerewe MINI Market

Ukerewe MINI Market We are dealies with home needs products

03/11/2025

NDUGU WA TANZANIA.
*Poleni sana mliopoteza ndugu jamaa na marafiki, poleni wa Tanzania 🇹🇿 wenzangu kwa ujumla tumepata kovu lisilo sahaulika vizazi na vizazi.*
Mungu wa Mbinguni atutie nguvu katika hali hii Tunayoipitia sasa!!
Amen🙏

16/10/2025

Nimeipenda hii analysis

15/10/2025

Msanii Wa Kizazi Kipya Barnaba Atimiza Miaka 50
Si Mchezo Ukimuona K**a Wa Miaka 30 kumbe 🙌🙌

17/09/2024

"*Sifa za Kiongozi Bora: Shika Zitakusaidia🤏*
___________________

1. Kiongozi bora ni mjuzi, siyo mjuaji. Mjuzi ni muelewa. Mjuaji ni mbabaishaji! Chenga!

2. Anaishi kwa maono na siyo maneno! Maono ni kuona kesho ukiwa leo! *Maneno ni hali ya kuwapotezea watu muda!*

3. Anaishi kwa mipango thabiti, siyo mipango ya ghafla k**a chafya! *Mipango ya ghafla hufanywa na watafuta kiki!*

4. Ni mtumishi wa watu siyo tishio la watu! Anajali utu kuliko vitu. *Haogopwi, anaheshimika!*

5. Yuko mbele katika kutafuta na nyuma katika kula. *Anakula baada ya watu wake kushiba!*

6. Anafundisha watu wake kuvua samaki na siyo kupokea samaki. *Vya kupewa hulemaza akili!*

7. Ni jasiri siyo jeuri! Ujasiri ni unyenyekevu. *Unyenyekevu siyo kujikomba!*

8. Anajiamini kwa sababu anajua kuna maisha baada ya uongozi. *Hababaiki na cheo. Ukipata nafasi poa, akikosa sawa tu, hajisikii kufakufa😄!*

9. Kiongozi bora hafanyi maamuzi magumu anafanya maamuzi sahihi. *Maamuzi magumu ni kukomoana!*

10. Kiongozi bora ana utulivu wa mwili na akili. *Hakurupuki katika kutenda na kusema na kujibu!*

11. Anaamini na kufanya maamuzi kwa tafiti na siyo hisia! Anaongozwa na Falsafa ya *No research no right to speak na siyo umbea na majungu!*

12. Anaona majibu katika kila changamoto na siyo changamoto kwa kila majibu!

13. Ni mkubwa kuliko changamoto za jamii. Linapotokea tatizo halalamiki na watu wake, wala hashangai na watu wake. *Analimaliza na watu wake!*

14. Ni muungwana siyo mshenzi! *Mshenzi ni sawa na pembe la ng'ombe hata ukilifunika kwa kanga utalijua tu.*

15. Ana masikio makubwa na mdomo mdogo. Anasikiliza sana na kuongea kidogo! *Mungu alitupa mdomo mmoja na masikio mawili ili tusikie sana na kuongea kidogo*.

16. Ni mbunifu siyo muigizaji. Anafanya kazi kuacha alama na siyo kuacha laana!

17. Anajipenda, hajipendelei. Kujipenda siyo kujipendelea! *Chukua hii!*

18. Anatumia kichwa kufikiri siyo tumbo! *Tumbo hushawishi wizi!*

19. Kiongozi bora siyo umri bali hekima na maarifa! *Maarifa ni nini unajua, hekima ni wakati gani useme unachokijua!*

20. Ni kioo cha jamii siyo kituko cha jamii! Kituko ni kituko tu. *Unajilimbikizia mali za umma ukifa unaziacha. Wewe ni kituko!"*

21. Anajali wengine na siyo kujijali yeye na kutanguliza Maslahi yake binafsi.

22. Ni mzalendo kwa vitendo na si maneno tupu.

23. Anae wapenda anao waongoza na kuwaogopa wanao jipendekeza kwake.

24. Awe mweledi, Mchapa kazi na mwadirifu katika Utumishi wake

25. Awe mtiifu kwa viongozi wake wa juu na mtiifu kwa anawaogoza.

26. Awe mvumilivu na si mropokaji na Awe mtu wa kufuata kanuni, taratibu, Sheria na Katiba ya Nchi au ya Taasisi anayotumikia. Amen 🙏🙏🤲

Address

ILOMBA-CCM AREA

025

Opening Hours

Monday 08:00 - 23:00
Tuesday 08:00 - 23:00
Wednesday 08:00 - 23:00
Thursday 08:00 - 23:00
Friday 08:00 - 23:00
Saturday 09:00 - 23:00
Sunday 09:00 - 23:00

Telephone

+255755990220

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ukerewe MINI Market posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ukerewe MINI Market:

  • Want your business to be the top-listed Grocery Store?

Share