26/11/2025
KABLA HUJAANZA UFUGAJI WA NGURUWE, FAHAMU UKWELI HUU.
Watu wengi huingia kwenye ufugaji wa nguruwe wakidhani ni biashara rahisi na ya kupata pesa haraka. Wengine hata hukopa ili waanze. Baada ya miezi miwili, malalamiko yanaanza.
Ukweli ni kwamba ufugaji wa nguruwe ni mzuri — lakini tu k**a unaujua vizuri. Hebu nikuambie k**a mtu ambaye amepitia huko.
1. Chakula ndicho changamoto yako kubwa.
Usidanganywe. Gharama ya chakula ndiyo itakula fedha zako nyingi. Bila mpango mzuri, unaweza kuingia kwenye madeni. Nguruwe wanaweza kukuingiza hasara haraka k**a huna nidhamu ya kulisha.
2. Huwezi kuwa msafiri wa mara kwa mara.
Nguruwe hula kila siku bila kukosa. Ukiacha kulisha siku moja tu, utaona madhara. K**a unafikiri unaweza kuwaacha bila uangalizi, utashangaa.
3. Joto linaweza kuharibu kila kitu.
Wakati wa joto kali, nguruwe hupunguza ulaji wa chakula na wengine hufariki kimya kimya. Jenga banda lenye hewa safi na uwape maji ya baridi na safi muda wote. Joto huua zaidi kuliko magonjwa.
4. Harufu si rafiki.
Ukishindwa kusimamia uchafu na maji taka, utachukia shamba lako na majirani watakuchukia zaidi. Fanya mipango ya mifereji na mfumo wa usafi kabla hujaweka nguruwe.
5. Magonjwa hayatoi taarifa.
Nguruwe wakipata ugonjwa, huenea kwa kasi. Safisha banda mara kwa mara na usiruhusu watu kuingia ovyo. Nunua nguruwe wenye afya — si wale wa bei ya kutisha ambao huleta matatizo.
6. Nguruwe hawakui kwa kasi sawa.
Hata ukiwalisha chakula kilekile, utakuta baadhi wanakua haraka na wengine polepole. Usipanic — fuatilia afya zao, deworm, na hakikisha wote wanapata chakula cha kutosha.
7. Bei ya soko hubadilika bila kutarajia.
Unaweza kuwalea kwa miezi, halafu unauza kwa hasara. Huu ni ukweli ambao wengi hawasemi. Unaweza tu kujiandaa na kuwa na mpango B.
8. Usiwaamini wafanyakazi kupita kiasi.
Wengine hupoteza chakula, kuuza nguruwe kwa siri, au kuficha taarifa muhimu. Hakikisha unafanya ukaguzi binafsi mara kwa mara. Macho yako ndiyo mfanyakazi wako bora zaidi.