28/04/2026
NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe: 28/04/2026
SOMO: NENO LA MUNGU LIKIKOSEKANA NDANI YAKO NI RAHISI KUMKOSEA MUNGU
Zaburi119: 11 "Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako, nisije nikakutenda dhambi"
Wewe uliyemwana wa Mungu unapaswa kuliweka Neno la Mungu moyoni mwako ili uwe salama. Haiwezekani umuombe Mungu juu ya kupata mtaji wa biashara yako halafu shetani aje kuchezea biashara yako mpaka inakufa.
Wewe uliye na Neno la Mungu ndani yako haiwezekani shetani aje achezee ndoa yako mpaka ivunjike, ukiona hivyo tambua kuwa kuna mahali hautendi sawa sawa; kwa maana Kristo akiwa ndani yako inamaana kuwa Nuru ipo ndani yako hivyo giza haliwezi kukaa kwako.
K**a Neno halipo ndani yako ni rahisi kumtenda Mungu dhambi. Neno haliwezi kukaa kwako k**a Yesu hayupo ndani yako kwa sababu Yesu na Neno ni mmoja. Yesu akiwa ndani yako maana yake Neno lipo ndani yako na Neno likiwa ndani yako wewe utazaa matunda.
Sauli alimkosea Nabii wa Bwana Samweli mara mbili kwa kukosa adabu matokeo yake akaangamizwa. Kuna watu wengine wanasema wameokoka lakini wanakosa adabu mbele za Mungu, hawamuheshimu Mungu tena kwa maana wanawadharau Watumishi wa Mungu.
Usipokuwa na adabu na kuwa mtii kwa Mtumishi aliyepakwa mafuta na Mungu na kuwekwa mbele yako ili kukuongoza basi huyo Mtumishi anao uwezo mkubwa wa kukuondolea talanta yako, nafasi yako na baraka zako.
Mungu akusaidie kuelewa hii siri uweze kufikia malengo ya kuumbwa kwako. Natamani wanangu mfike mahali pa kushangilia baraka zenu; lakini k**a utakuwa siyo mtii na utakosa adabu utamfanya Mungu asisikie maombi yako.