Muhammad -saww- Mtume wa Umma

Muhammad -saww- Mtume wa Umma Uislamu ni Dini ya Amani, Dini ya Haki, Usawa na Uadilifu.

🎥📸🇮🇷Maafisa na Mawaziri wa Iran Washiriki Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds Mjini Tehran🔻 Maafisa na mawaziri kadh...
13/03/2026

🎥📸🇮🇷Maafisa na Mawaziri wa Iran Washiriki Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds Mjini Tehran

🔻 Maafisa na mawaziri kadhaa wa Iran wameshiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaliyofanyika katika Mji Mkuu Tehran, wakijiunga na maelfu ya wananchi waliokusanyika kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina.

2️⃣ABNA NEWS -SWAHILI💠
👇🏾
📢Sauti ya Wasiokuwa na Sauti
⬇️
https://whatsapp.com/channel/0029VbCfXCL3LdQQnHHI6i1K

🕌🤲🏾   wamefanya ibada na a’mali mbalimbali katika kuhuisha Usiku Mtukufu wa Tatu wa Laylatul Qadr (Usiku wa Makadirio) ....
13/03/2026

🕌🤲🏾 wamefanya ibada na a’mali mbalimbali katika kuhuisha Usiku Mtukufu wa Tatu wa Laylatul Qadr (Usiku wa Makadirio) ... Na kuiombea Ushindi pamoja na Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon katika Mapambano yao Haki dhidi ya Batili.

2️⃣ABNA NEWS -SWAHILI💠
👇🏾
Sauti ya Wasiokuwa na Sauti
⬇️
https://whatsapp.com/channel/0029VbCfXCL3LdQQnHHI6i1K

Sayyid Ali Khamenei: Sisi sio watu wa kwenye mahandaki
12/03/2026

Sayyid Ali Khamenei: Sisi sio watu wa kwenye mahandaki

17/01/2026
16/01/2026
Samehe waliokukosea
07/01/2026

Samehe waliokukosea

Kauli ya Imam Baqir (as) -

  (a.s)Katika ulimwengu wa Kiislamu hakukuwa na mtu yeyote aliyemzidi Imamu Ali bin Abi Talib (a.s.) katika fadhila, eli...
07/01/2026

(a.s)

Katika ulimwengu wa Kiislamu hakukuwa na mtu yeyote aliyemzidi Imamu Ali bin Abi Talib (a.s.) katika fadhila, elimu, jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na sifa zote za juu za kibinadamu, isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (s.a.w.w.).

Imamu Ali (a.s.) alikuwa mwenye elimu pana zaidi, shujaa kuliko wote, mcha Mungu wa kweli, na mwenye kutoa hukumu kwa haki zaidi miongoni mwa Masahaba. Alikulia katika malezi ya Mtume (s.a.w.w.), akajifunza kutoka kwake moja kwa moja, hivyo akawa mtu wa karibu zaidi naye kielimu, kimaadili na kivitendo.

Alishiriki katika vita vyote muhimu vya Uislamu, akabeba bendera ya haki katika nyakati ngumu, na upanga wake ukawa ngao ya kuilinda Dini ya Mwenyezi Mungu. Elimu yake ikawa nuru kwa Umma, na uadilifu wake ukawa kipimo cha haki.

Waislamu, licha ya tofauti za kimadhehebu, wameafikiana juu ya utukufu wa daraja lake na ukubwa wa nafasi yake, na kwamba Imamu Ali (a.s.) ni kielelezo kamili cha mwanadamu bora baada ya Mtume (s.a.w.w.).

Amani iwe juu yake siku alipozaliwa katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu, siku alipopigania haki kwa subira, siku alipoaga dunia shahidi katika mihrabu ya ibada, na siku atakapofufuliwa akiwa hai.

🎙️FADHILA ZA SAYYIDAT FATIMA (S.A) - Binti Kipenzi wa Mtume (s.a.w.w)💐🌺Katika tukio maarufu lililonukuliwa na vitabu vya...
10/12/2025

🎙️FADHILA ZA SAYYIDAT FATIMA (S.A) - Binti Kipenzi wa Mtume (s.a.w.w)

💐🌺Katika tukio maarufu lililonukuliwa na vitabu vya historia na hadith, Bibi Fatima (s.a) alienda kwa uchungu mkubwa kuondoa matumbo ya ngamia yaliyowekwa na washirikina kichwani mwa Mtume (s.a.w.w) wakati akiwa katika sajda. Tukio hili linabaki kuwa ushahidi wa mapenzi yake ya kipekee na ulinzi usioyumba kwa Mtume wa Uislamu(s.a.w.w).

📡🎥🌺Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Hadithi za maisha ya Bibi Fatima Zahraa (a.s) zimejaa mifano ya upekee wa imani, ujasiri na mapenzi ya dhati kwa Baba yake, Mtume Muhammad (s.a.w.w).

📡🎥💐Habari Kamili 👇🏾

Katika tukio maarufu lililonukuliwa na vitabu vya historia na hadith, Bibi Fatima (a.s) alienda kwa uchungu mkubwa kuondoa matumbo ya ngamia yaliyowekwa na washirikina kichwani mwa Mtume (s.a.w.w) wakati akiwa katika sajda. Tukio hili linabaki kuwa ushahidi wa mapenzi yake ya kipekee na ulinzi usioy...

"Marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.”Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa au upweke,...
02/12/2025

"Marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.”

Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa au upweke, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, walio tayari kumpokea katika safu yao.

📡🎥 Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt(as)-ABNA- Mashahidi wa Uislamu halisi hawapati upweke katika safari yao ya haki; hata pale wanapokuwa mbali,katika ugeni,au katika mazingira magumu yanayoonekana kana kwamba hayana msaada.

Ugeni kwao si mwisho wa njia,bali ni mwanzo wa kuungana kwa kina na msafara wa watu wa haki waliotangulia, Mitume, Manabii, Maswali na Waumini vipenzi wa M/Mungu.
-
📡🎥Habari Kamili⬇️

"Katika ugeni hakuna hofu ya upweke; marafiki wapendwa wako wengi zaidi upande ule mwingine.” Kwa maana kwamba: Shahidi anapovuka kutoka dunia hii, haogopi kutengwa, kwa sababu anatambua wazi kuwa upande wa pili kuna kundi kubwa la wacha-Mungu, wakweli, watu wema, na mashahidi waliomtangulia, wali...

✍🏽Adabu Muhimu Miongoni mwa Adabu za Kusoma Qur’an Tukufu📖Qur’ani si kitabu cha kusomwa kwa macho na kufahamika kwa fikr...
29/11/2025

✍🏽Adabu Muhimu Miongoni mwa Adabu za Kusoma Qur’an Tukufu

📖Qur’ani si kitabu cha kusomwa kwa macho na kufahamika kwa fikra pekee. Qur’ani ni minong’ono ya Mola kwa nyoyo zilizo na masikio ya roho. Adabu ya tilawa si sura za nje tu; adabu ya kusoma Qur’ani ni kutambua kuwa umeingia katika uwepo wa Allah, na kwamba kila aya ni pumzi kutoka kwa Mola wa walimwengu, na wewe ndiye unayeambiwa.

📡🎥Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt(as)-ABNA- *Usiku wa maneno, katika kimya ambacho hata nyota hazinong’onezi, Aya moja katika Suratul-Qasas ilinivuta:

«فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِیَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَیْمَنِ فِی الْبُقْعَةِ الْمُبَارَکَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن یَا مُوسَیٰ إِنِّی أَنَا اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِینَ»

📡⬇️

Qur’ani si kitabu cha kusomwa kwa macho na kufahamika kwa fikra pekee. Qur’ani ni minong’ono ya Mola kwa nyoyo zilizo na masikio ya roho. Adabu ya tilawa si sura za nje tu; adabu ya kusoma Qur’ani ni kutambua kuwa umeingia katika uwepo wa Allah, na kwamba kila aya ni pumzi kutoka kwa Mola wa...

Address

Qom
0098

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Muhammad -saww- Mtume wa Umma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category